Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amewataka viongozi kuzingatia maslahi ya wananchi kama njia moja ya kumarisha maendeleo ya jimbo akihoji kuwa jimbo la Nakuru haliwezi kuendelea na fujo na siasa za mara kwa mara.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vile vile  gavana huyo amewashukuru viongozi wale ambao wanatekeleza wajibu wao katika jimbo hilo akisema kuwa ni njia moja ya kuimarisha uchumi wa kaunti hiyo na nchi ya kenya kwa ujumla.

Matamshi yake yameungwa mkono na mbunge wa Nakuru Magharibi Samwel Arama ambaye amesema kuwa anaunga mkono hatua ya serikali ya jimbo la Nakuru ya kuwaondoa wachuuzi katikati mwa mji huo.

Kinuthia pia amepuuzilia mbali kikao kilichofanyika mwishoni mwa wiki jana kati ya mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria na mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri akidai kuwa viongozi hao wamebuni mikakati mpya ya kuwaleta viongozi kutoka maeneo ya nje kutoa suluhu kwa maswala yao ya kisiasa katika jimbo hilo.

Huku akiguzia kuhusu kikao hicho kilichohudhuriwa na wabunge Moses Kuria, David Gikaria na Kimani Ngunjiri gavana Kinuthia ametaja hatua hiyo kama ya aibu kubwa akiongeza kuwa wakati umefika kwa wabunge wa Nakuru    kuzingatia maswala yanayohusu maeneo yao kuliko kujihusisha na siasa zisizo na maana ambazo amehoji kuwa zitalemaza maendeleo.