Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amelalamikia muonekano wa kigeographia katika mji wa Nyamira kama kikwazo cha ustawi wa kaunti hiyo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiwahutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya Jumatano, Nyagarama alisema kuwa jinsi ujenzi wa mji huo ulivyojengwa miaka kadhaa iliyopita ni njia mojawapo inayozuia wawekezaji wengi kuekeza katika kaunti hiyo. 

"Kikwazo kikuu ambacho tunakabiliana nacho hasa kwa kustawisha mji huu kimaendeleo ni jinsi mji huu ulivyojengwa siku za hapo nyuma, kwa maana hatuna majumba ya kibiashara ili wawekezaji kuekeza," alisema Nyagarama. 

Nyagarama aidha alisema kuwa kutokana na hali hiyo, serikali yake imeweka mikakati ya kuona iwapo jiji la kisasa litajengwa katika eneo la Nyamaiya ama Sironga ili kuwavutia wawekezaji. 

"Kwa sababu kuwa mji huu wa Nyamira haukujengwa kwa njia ambayo inaweza waruhusu wawekezaji hasa wa maduka ya kijumla kuekeza hapa sasa tumeweka mikakati ya kuona iwapo tutajenga jiji jipya kule Sironga ama Nyamaiya kulingana na uwepo wa ardhi ili kuwavutia wawekezaji zaidi," aliongezea Nyagarama.