Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama ameyashtumu mauaji ambayo yalitekelezwa katika wadi ya Bokeira siku ya Jumamosi wiki jana.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana huyo ambaye alizuru eneo hilo siku ya Jumatatu alionekana mwenye huzuni mwingi na hasira, kwa mauaji ya mme na mke wake katika familia moja huku wanao wakiachwa na majeraha.

"Nimekerwa sana na mauaji haya ambayo yametekelezwa hapa katika wadi hii ya Bokeira. Ningependa maafisa wetu wa CID wafanye uchunguzi kwa kina hadi wawatie mbaroni majangili hawa ambao wametekeleza unyama huu," alisema gavana Nyagarama. 

Pia gavana huyo alisema kuwa atagaramia vitu vyote vilivyoteketezwa na magaidi hao katika nyumba hiyo, kando na kutoa changamoto kawa vijana waache kujihusisha na mambo ya uhalifu.