Hospitali ya kiwango cha nne ya Oresi iliyoko mjini kisii imepata afueni baada ya gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae kuahidi kuinunulia hospitali hiyo shamba.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumatatu katika hafla ya kusherekea siku ya Madaraka, gavana Ongewae alisema serikali yake itainunulia hospitali hiyo ya Oresi shamba kubwa kwani hospitali hiyo iko katika shamba ndogo.

“Serikali yangu itainunlia hospitali ya oresi shamba kubwa maana shamba inayotumika kwa sasa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya hospitali hiyo. Hospitali hiyo inahitaji kuongeza majengo ya kuwahudumia wagonjwa,” alisema Ongwae.

Wakati huo huo, gavana Ongwae alisema kitengo cha kuwahudumia wagonjwa katika hospitali za kisii kitainuliwa zaidi ili wagonjwa wawe wanahudumiwa hadi kiwango kinachohitajika.

“Serikali yangu itahakikisha wagonjwa wanapata huduma bora wanapoenda katika hospitali za kaunti hii. Dawa zitaongezwa kwa kila hospitali ili kila mwananchi apata haki yake anapohudumiwa,” aliongezea James Ongwae.

Ongwae aliitaka serikali ya kitaifa kuongeza pesa katika sekta ya afya jinsi ilivyokuwa hapo mbeleni huku akisema sharti hospitali za kiwango cha tano na sita zipate pesa nyingi.

“Kuna baada ya vitu ambavyo havijashughulikiwa na serikal ya ugatunzi haswa kwa sekta ya afya maana hakuna pesa za kutosha kwa sekta hiyo,” alidokeza ongwae.

Aliongezea: “Naomba serikali ya Kitaifa kuongeza pesa zaidi katika sekta ya afya ili vitu zote kushughulikiwa kikamilifu na serkali za kaunti.”