Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema serikali yake imetenga pesa kwa ujenzi wa kiwanda cha majani chai ambacho kitajengwa eneo la Sombogo eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Ijumaa katika uga wa shule ya upili ya wasichana ya Marani,  katika sherehe ya mazishi ya Chrisantos Mekenye Omoi alliyekuwa mfanyikazi wa mbunge wa eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini, Ongwae alisema serikali yake imetenga shilling millioni 30 kwa ujenzi  wa kiwanda hicho.

Hii ni baada ya wakulima wa eneo hilo kusumbuka kwa muda mrefu kwa majani chai yao kuwa katika vituo kwa zaidi ya siku tatu mfululizo bila kuchukuliwa na kuwasababishia wakulima hasara nyingi kupita kiasi.

“Serikali yangu imeweka mikakati ya kujenga kiwanda cha majani chai katika eneo la Sombogo maana wakulima wa eneo hili wamesumbuka sana kwa kupata hasara kwa kutochukuliwa kwa majani chai yao,” alisema Ongwae.

Aidha gavana huyo alisema atashirikiana na viongonzi wote wa kaunti yake wakiwemo wabunge ili kukwamua miradi ambayo imekwama kuendelea ili maendeleo yafanyike zaidi katika kaunti yake.

Baadhi ya miradi aliyoahidi kukwamua ni mradi wa maji, ujenzi wa taasisi ya masuala ya afya katika hospitali zote za kaunti hiyo ya Kisii.

Sherehe hiyo ya mazishi iliuhudhuriwa na seneta mteule kutoka kaunti ya Kisii Hosea Ochwang, aliyekuwa mbunge wa Kitutu Masaba Walter Nyambati, mbunge wa kitutu chache kusini Richari Onyonga, mbunge Jimmy Angweny na viongonzi wengine ambao waliahidi kushirikiana na Ongwae kuleta maendeleo.