Gavana wa kaunti ya Lamu Issah Timamy amekashifu mpango wa usafari uliyoko kwa sasa ambapo abiria wanaotoka mjini Mombasa na kuelekea Lamu hulazimika kushuka katika kila kizuizui cha polisi na kufanyiwa upekuzi.
Kulingana na Timamy, hali ya usalama katika kaunti hiyo imeimarika lakini cha kustajabisha bado maafisa wa usalama wanafanyia upekuzi abira huku wahalifu wakishindwa kuwakabili.
Akizungumza katika kongamano la wadau mbalimbali wa kibiashara katika hoteli moja mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Timamy aliitaka serikali kubadilisha mipango ya usafiri ili kuepukana na usumbufu wa abiria.
“Tumechoshwa na idara ya polisi kuwahangaisha wakazi wa pwani wanaoabiri mabasi kuelekea Lamu kutoka Mombasa katika vizuizi ilhali,"gavana Timamy alisema.
Hatua hiyo imejiri licha ya kuwepo kwa msafara wa polisi unaoandamana na mabasi ya abiri kuelekea mjini Lamu kutoka mjini Mombasa.