Gavana James Ongwae amewaomba wakazi wote wa kaunti ya Kisii na vikundi mbali mbali kujiandikisha katika kaunti hiyo ili wasimamizi wa kaunti hiyo waweze kuweka mikakati ya kuwaafikia na kutoa funzo maalumu kwao jinsi ya kujiendeleza kimaisha.
Akiongea jana katika ukumbi wa kitamaduni mjini Kisii, wakati wa kujibu baadhi ya maswali yalikua yokiulizwa na wakazi walihoudhulia kikao hicho, alisema kuwa kuna umuhimu wa kujua baadhi ya vikundi mbali mbali ili kuwasaidia kutoa mafunzo maalumu kwao hasa jinsi ya kujua mipango ya serikali ya kaunti ya Kisii.
"kuna umuhimu wa Kujulisha na kufahamisha wakazi wote jinsi serikali imeweka mikakati yao kwa wakazi wao na hayo yatawezekana wakati tutatambua vikundi mbali mbali ili kurahisisha kuwafikia,” alihoji Ongwae
Ongwae alitaka makundi kama yale ya kinamama,wanabodaboda na sekta ya uchukuzi (matatu) kujiweka pamoja ili waweze kufikiwa na kupewa funzo maalumu jinsi ya kushirikian na kaunti na kijiimarisha kimaisha.
Aidha, aliwauliza mawaziri wake kuanza kutambua na kuandikisha makundi hayo kwa mafunzo hayo.
"Nawaamuliza mawaziri wangu wote wa kaunti kuanza kutambua na kuandikisha makundi hayo ili tuweze kupata idadi kamili na kupanga jinsi ya kuwafikia na kuanza kutoa mafunzo hayo," aliongezea Ongwae.
Haya yote ni kutokana na kulalama kwa baadhi ya wakazi wa kaunti ya Kisii, kuwa bado hawajafikiwa na kupata mafunzo hayo ili kujua ni yapi Serikali hiyo imepanga kuyatekeleza kwa wakazi wa Kaunti hiyo.
Kwingineko aliwaomba wakazi wote kushirikiana na serikali yake ili kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kuinua viwango vya maendeleo.
kulingana na Gavana Ongwae hata kama serikali ya kaunti ya Kisii iliorodheshwa kuwa la sita bora kati ya kaunti ambazo zimefanya bora alisema kuwa yeye atahakikisha kuwa kaunti ya Kisii inaorodheshwa ya Kwanza katika utafiti ujao.