Wazazi wa kaunti ya Kisii wana kila sababu ya kutabasamu baada ya gavana wa kaunti ya hiyo James Ongwae  kuahidi kuongeza pesa za kusaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kulipa karo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea siku ya Jumanne  katika mji wa Kisii gavana Ongwae alikiri kuwa pesa za ufadhili katika bajeti ya 2015/2016 zitaongezwa  hadi shillingi millioni tano kwa kila wadi.

“Tunataka kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amepata fursa ya kusoma ili tupandishe viwango vya elimu katika eneo hili letu,” akasema Ongwae.

 “Mwaka uliopita kila wadi ilipokezwa millioni moja mwaka huu tulikaa chini na wawakilishi wa wadi katika kaunti yangu tukaelewana kuwa tutaongeza pesa za ufadhili,” akasema Ongwae.

 “Nilazima tuinue viwango vya elimu katika kaunti hii. Hatua hii itasaidia kuinua kiwango cha maendeleo katika eneo hili,” akaongeza Ongwae.

Wakati uo huo,gavana alisema kiini cha kuongeza pesa hizo kila wakati ni kufuatia changamoto za umasikini na ongezeko la wanafunzi mayatima.