Shughuli za kawaidwa zilishitishwa kwa takriban dakika thelathini katika eneo la Kisauni siku ya Alhamisi baada ya vijana waliokuwa wamejihami kwa panga kujitokeza barabarani huku wakilalamikia kuhangaishwa na maafisa wa polisi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana hao ambao wanahusishwa na kundi ya wahalifu la wakali kwanza walizuia barabara zote na kusimamisha magari ambayo yalikuwa yakipita kuelekea katikati mwa mji wa Mombasa.

Aidha maduka yote katika eneo hilo yalilazimika kufungwa huku kila mmoja akihofia usalama wake licha ya kuwa hakuna mtu yeyote aliyepata majeraha katika hali hiyo.

Hata hivyo maafisa wa polisi walifika kwa wakati na kuwatawanya vijana hao huku wakiendelea na msako wa kuwakamata wanagenge hiyo la wakali kwanza.