Mbunge wa eneo bunge la Mugirango Magharibi James Gesami amejitoza rasmi kutangaza azma yake yakuwania ugavana katika kaunti ya Nyamira.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wanahabari kwenye parukia la kanisa katoliki kule Nyamira baada yakuhudhuria hafla yakuchangisha pesa zakuwajengea watawa makao rasmi, Gesami alisema shinikisho za wakazi wa Nyamira zimemlazimu kujitosa ulingoni.

"Ni shukurani kubwa kwa wakazi wa eneo bunge la Mugirango Magharibi kwa kunipa nafasi ya kuwahudumia kwa mihula miwili mtawalia na kwa sasa nimejotoza rasmi kwenye kinyanganyiro cha ugavana kwa sababu ya shinikizo za wakazi wa kaunti hii." Gesami alisema.

Gesami aidha aliishtumu serikali ya gavana Nyagarama kwa utendakazi duni huku akihoji kuwa serikali ya kaunti hiyo imekuwa ikijishughulisha na ufujaji wa pesa za umma. 

"Nina hakika kuwa wakazi wa kaunti hii watanipa nafasi yakuwahudumia kama gavana wao kwenyw uchaguzi mkuu ujao kwa maana kwa miaka minne tangu serikali iliyopo ilipoingia mamlakani hatujaona miradi yeyote ya maendeleo ikitekelezwa ila uvujaji wa pesa za umma," aliongezea Gesami.