Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria ameahidi kuandaa sherehe kubwa ambapo fahali 50 watachinjwa iwapo mahakama ya kitaifa ya jinai, ICC itasitiza kesi dhidi ya naibu rais, William Ruto na mwanahabari Joshua arap sang.
Gikaria aidha alisema kuwa ana imani kwamba mahakama hio itamwaachilia huru Ruto na Sang.
"April 5 itakua siku kuu kwetu maana kitu ambacho tunatarajua si kingine ile kuachiliwa huru kwa Ruto, itakuwa siku kuu kwa wakenya," Gikaria alisema.
"Tayari nimewanunua fahali 50 wa kusherehekea uamuzi huo," Gikaria alisema.
Jumatano, mawakili wa Ruto na sang walitangaza kuwa mahakama hio imetenga April 5, kama siku ya kutoa uamuzi wake wa kutokuwa na kesi dhidi ya wawili hao.
Iwapo majaji wataamua wawili hao hawana kesi, basi utakua mwisho wa kesi hio na mawakili wa Ruto na Sang watatakiwa kuwaita mashahidi wao iwapo Mahakama itaamua kuwa wawili hao wana kesi ya kujibu.
Ruto na Sang wanashtakiwa na madai ya kuhusika na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo takriban watu 1500 walifariki na wengine wengi kufurushwa makwao. Gikaria aliyasema haya siku ya jumanne akiwahutumbia wananchi mjini Nakuru.