Mbunge wa Nakuru mjini David Gikaria amepinga vikali pendekezo lililotolewa na afisa mmoja wa kaunti ya Nakuru kwamba miili ya wafu ichomwe kutokana na ukosefu wa ardhi ya kuzika wafu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika kikao na wanahabari Nakuru Jumatano, Gikaria ambaye wakati mmoja alikuwa Meya wa Nakuru alisema kuwa swala la mili kuchomwa si suluhu mwafaka Kwa ukosefu wa makaburi bali serikali ya kaunti inafaa kutenga fedha katika bajeti na kununua ardhi.

"Hili swala linaweza tu tatuliwa iwapo serikali ya kaunti ya Nakuru itanunua ardhi mbadala ya kutumika katika kuwazika wafu,"alisema Gikaria.

Wakati huo huo, alitoa wito kwa wakaazi wa Nakuru kuzingatia kuwazika wafu katika maeneo yao ya mashambani.