Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria ametangaza kuwa atawania tena nafasi ya ubunge kwenye uchaguzi ujao wa mwaka wa 2017.

Gikaria alisema hayo alipokuwa akizungumza katika bustani siku ya Jumannne, katika hafla ya kutoa hundi ya shilingi milioni 25 kwa wanafunzi kutoka jamii maskini.

Wakati huo huo, Gikaria pia alimpigia debe gavana Kinuthia Mbugua akiwataka wakaazi wa Nakuru kumpigia kura katika nafasi ya ugavana kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Tayari baadhi ya viongozi wamejitokeza kuweka bayana kwamba watawania kiti cha ugavana katika kaunti ya Nakuru kwenye uchaguzi mkuu ujao ikiwa ni pamoja na mweyekiti wa halmashauri ya usafiri na usalama wa barabarani nchini NTSA Lee Kinyanjui na mwenyekiti wa mamalaka ya kudhibiti utumizi wa mihadarati na Pombe NACADA John Mututho.