Mwenyekiti wa chama cha TNA kaunti ya Nakuru Samuel Githaiga ametoa with kwa viongozi kaunti ya Nakuru kuwajibika na kuacha siasa za ukabila na mgawanyiko.
Katika kikao na wanahabari mjini Nakuru jumstano,Githaigs amesema kuwa no jambo la kusikitisha kwa viongozi kuendeleza siasa za ukabila.
''Tunajua kaunti ya Nakuru ina makabila yote vivo basis viongozi hawafai kueneza siasa za ukabila," Githaiga alisema.
Wakati huo huo Githaiga aliwataka wakaazi wa kaunti ya Nakuru kuwspiga msasa viongozi kabla ya kuwachagua akisema kuwa baadhi ya viongozi wamezembea kazini.
Vilevile, aliwasuta viongozi wanaosabsbisha migogoro ndani ya TNA Nakuru.