Shirika la Greenbelt Movement limeanzisha mpango wake kote nchini unaonuia kuwahimiza vijana kutunza na kuimarisha talanta zao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Teresa Maina ambaye ni afisaa mkuu wa maswala ya jinsia katika shirika hilo aliyeongea katika hafla ya maonyesho ya talanta mjini Nakuru mwishoni mwa wikendi hii alisema kuwa iwapo talanta zaweza kulindwa, watoto wanaweza kuimarika kimaadili na katika Nyanja tofauti tofauti na kulisaidia taifa la Kenya kuafikia malengo yake.

“Vijana wengi tunazo talanta na ikiwa tutazidhamini na kuzienzi basi pia taifa litasonga mbele na kufanikiwa pakubwa,” Maina alisema.

Alisema kuwa katika vikao vyao kama hivyo wanasisitiza haja ya kuwepo kwa uwiano sawia na amani miongoni mwa vijana.