Mkurugenzi wa Shirika la Haki Africa Hussein Khalid katika hafla ya awali. Ametishia kuishtaki serikali kwa kukandamiza haki na uhuru wa Wakenya wa kupata matibabu. Picha/hrw.org

Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika la Haki Afrika limeitaka serikali kutatua mgomo wa madaktari ambao umelemaza shughuli za afya kote nchini.

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, katibu wa shirika hilo Hussein Khalid, alisema amegadhabishwa na hatua ya mahakama kuwafunga jela kwa mwezi mmoja wakuu wa chama cha madaktari KMPDU.Khalid alisema kuwa hiyo sio suluhisho ya kumaliza mzozo huo bali ukiukaji wa haki za madaktari.Aidha, ametishia kuishtaki serikali kwa kuwanyima Wakenya haki yao ya matibabu.“Tutaelekea mahakamani kuishtaki serikali kwa kukandamiza haki na uhuru wa Wakenya wa kupata matibabu,” alisema Khalid.Kauli hii inajiri baada ya mahakama ya masuala ya ajira kuwahukumu viongozi saba wa chama cha madaktari kifungo cha mwezi mmoja jela, baada ya kushindwa kusitisha mgomo huo ambao umedumu kwa zaidi ya miezi miwili.Jaji Hellen Wasilwa amesema hakuna sababu ya kutosha kuonyesha ni kwa nini madaktari hawajasitisha mgomo huo.Aidha, ameamuru mazungumzo ya kumaliza mgomo huo yaendelee.Hapo awali, Jaji Wasilwa alikuwa amewapa viongozi hao muda wa wiki mbili kumaliza mgomo huo, na baadaye akawaongezea siku tano.

Madaktari kwa upande wao wanaitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara.