Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika limekashifu vikali ziara ya wiki tatu ya wabunge 12 kuelekea Rio kushudia michezo ya Olimpiki.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Shirika hilo, kupitia afisa wake Francis Gamba, limeitaja safari hiyo kama utumizi mbaya wa fedha za umaa, ikizingatiwa bado Wakenya wanakumbwa na matatizo ya uchumi.

Ameongeza kuwa ingekuwa bora iwapo pesa hizo zingetumiwa kuendeleza maendeleo muhimu nchini kama vile kusaidia watoto wanaorandaranda mitaani.

“Safari hiyo haina manufaa yoyote bali ni kutumia pesa za mlala hoi bure,” alisema Gamba.

Taifa la Kenya limetuma wabunge 12 nchini Brazil kuhudhuria michezo inayoendelea kwa sasa.

Safari nzima ya wabunge hao 12 itaigarimu serikali shilingi milioni 8.4 ambazo ni pesa za umma.

Kila mbunge atapokea marupurupu ya shilingi elfu 50 kila siku.

Aidha, kila mbunge atatumia tiketi ya ndege ya shilingi 259,711 ambapo wabunge wote 12 watatumia kima cha shilingi milioni 3.12.