Serikali imetakiwa kutoa haki kwa waathiriwa wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Kauli hii ilitolewa siku ya Jumatano na mkurugenzi mkuu wa shiriki la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika, Hussein Khalid.
Khalid alisema wale walioathiriwa ni lazima waweze kupata haki yao na wale waliohusika na machafuko hayo waweze kupatikana ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wakati huo huo, amewataka wakenya kuepuka kujigawanya kwa mirengo ya kisiasa kufuatia uamuzi huo na badala yake kuangaliwa maswala ya kujenga nchi na kusahau yaliyopita.
Kauli hii inajiri baada ya mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kutoa uamuzi wa kutokuwa na kesi ya kujibu kwa naibu rais William Ruto na aliyekuwa mwanahabari Joshua Arap Sang siku ya Jumanne.