Hakimu Henry Nyakweba ameshutumu baadhi ya wanahabari kwa kuandika habari za kupotosha.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Nyakweba alionekana kutopendezwa na jinsi wanahabari walivyoripoti kuhusu kesi moja ambapo washukiwa watatu wanatuhumiwa kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 13.

"Wanahabari munauhuru wa kutoa habari lakini ziwe za kweli na wala sio za kupotosha, kwani mwaweza haribu amani kwa muda mfupi. Taarifa zilizoandikwa kuambatana na kesi hii zinatoa twasira tofauti na mambo jinsi yalivyo,” alisema Hakimu Nyakweba.

“Mahakama haijaahirisha kusikiliza kesi hii kwa kukusudia kama ilivyoripotiwa. Upande wa kuendesha mashtaka ndio umechelewa na wala sio mahakama, kwa hiyo nawaomba muwe makini,” aliongeza.

Aliwataka wanahabari kutopaka idara ya mahakama tope kwa madai ya kuchelewesha haki.