Hakimu mmoja katika Mahakama ya Mombasa amekataa kupingwa picha na kuoneshwa kwenye runinga.
Hakimu Emmanuel Mutunga, anayesikiza kesi ya ugaidi inayomkabili mke wa marehemu Aboud Rogo, amekataa kupigwa picha kwa sababu za kibinafsi ambazo amesema hatazisema.
Mutunga aliwaambia wanahabari kuwa hapendi kuonekana kwenye runinga wala gazeti.
“Tafadhali msinipige picha kwa sababu ambazo sitazitaja kwa sasa,” alisema Hakimu Mutunga.
Mke wa marehemu Sheikh Aboud Rogo, Haniya Said Saggar, alitiwa mbaroni siku ya Jumatano, akiwa nyumbani kwake huko Kanamai, Kaunti ya Kilifi.
Haya yanajiri baada ya Bi Saggar kudaiwa kuhusika na magaidi walioshambulia Kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa siku ya Jumapili.