Seneta wa Mombasa Hassan Omar akiwahutubia wanahabari hapo awali. Photo/ the-star.co.ke

Share news tips with us here at Hivisasa

Seneta wa Mombasa Hassan Omar ametupilia mbali madai kwamba kuna mvutano baina ya viongozi wa mrengo wa NASA.Akizungumza kwenye kikao na wanahabrai mjini Mombasa, Omar alisema kwamba habari na uvumi unaonezwa kuwa viongozi wa NASA tayari wamegawanya madaraka ni porojo.Omar alidai kuwa hiyo ni njama ya serikali ya Jubilee kuwachanganya wananchi.Omar, aidha alisema kuwa mrengo wa NASA umejipanga vilivyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti, huku akiwahimiza wafuasi wa mrengo huo kutoingiwa na hofu na badala yake kujitenga na siasa za propaganda ambazo huenda zikaleta mgawanyiko miongoni mwao.Wakati huo huo, Omar ameitaka serikali ya Jubilee kuendeleza kampeni zake katika njia ya kuleta Wakenya pamoja na kuonya dhidi ya kueneza uvumi miongoni mwa wananachi.Hata hivyo, Omar alisema kuwa yuko tayari kumuunga mkono kiongozi yeyote wa NASA atakaye pewa wadhifa wa kupeperusha bendera ya urais kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti.