Mwenyekiti wa kampuni ya maji katika eneo la Kisii (Gusii water and sanitation company) Zachary Moguche amewahakikisha wakaazi wa mji huo na viunga vyake kuwa wataanza kupata maji kuanzia siku ya Jumatatu bila kukosa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni baada ya mji huo na vyunga vyake kukosa maji kwa wiki moja mfululizo kutokana na changamoto za kifedha huku akisema serikali ya kaunti hiyo imewalipa deni la shilingi millioni 3 kati ya millioni 5 ambazo ilikuwa nazo kama deni na kusema sasa maji hayatakosa kamwe.

Kulingana na mwenyekiti huyo, GWASCO  imeweka mikakati kapambe ya kuhakikisha maji hayakosi kwani maji ndio hutumika kwa kazi zote mjini humo.

Moguche alisema deni ambalo serikali ya kaunti ya Kisii ilikuwa nalo lilisababisha kampuni ya nguvu za umeme kukata stima katika eneo la Kegati ambalo hutumiwa kusambaza maji hayo.

“Nataka kusema kuwa serikali ya kaunti ya Kisii ilikuwa na deni la milioni tano na tayari wamelipa millioni tatu na sasa maji hayatakosa katika mji wa Kisii na vyunga vyake,” alisema Moguche.

“Naomba Wakaazi wa mji wa Kisii kutokuwa na mshangao, sasa maji yako na hamtasumbuka kwa ukosefu wa maji maana mikakati yote imeimarishwa,” aliongeza Moguche.