Maskwota wanaoishi katika shamba lenye utata la Waitiki sasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kuwathibitishia kuwa hawastahili kutoa ada yoyote ili kumiliki kipande cha shamba.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea katika hafla ya kisiasa katika eneo la Mtongwe, Joho alipinga matamshi yaliyotolewa na Rais Kenyatta kuwa maskota hao walipe shilingi laki 182 wakati wa ziara yake mjini Mombasa mwaka jana.

Wakiongea na mwandishi huyu baada ya hafla hiyo, Omar Zecha ambaye ni mkazi wa Likoni alisema kuwa amefurahishwa sana na mpango huo wa serikali ya kaunti ya mombasa ya kuwaondolea ada hiyo. 

"Kwa kweli tunamshukuru gavana wetu kwa kujitolea kututetea sie wanyonge. Miradi yetu mingi ilikuwa imekwama sasa tutajiendeleza," alisema Zuena Mrisa ambaye pia ni mkazi wa Likoni. 

Gavana Joho alisema kuwa ada hiyo sio halali kulipwa na maskota hao na kuwa serikali ya kaunti ya mombasa italishughulikia vilivyo swala hilo.