Gavana wa Mombasa Bwana Hassan Joho ametosha kuongoza Kenya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii sio kumlimbikizia sifa bure bali ni usemi ambao unaambatana na ukomavu wake kwenye ulingo wa kisiasa.

Hivi karibuni, Joho amewatia tumbo joto wapinzani wake.

Amekua mwandani wa karibu sana wa kigogo wa siasa Raila Odinga, al maarufu, Baba. Ametembea naye katika kila pembe ya taifa letu tukufu.

Joho anasikizwa toka magharibi hadi mashariki bila kusahau kusini hadi kaskazini.

Gavana huyu ana bidii katika chama cha ODM na hili limemfanya kupewa wadhifa mkuu chamani humo.

Tazama juhudi zake za kutuliza mawimbi ya siasa eneo la magharibi na utapenda ukakamavu wake.

Hatahivyo, Joho amekua na changamoto si haba ambazo anadai ni mbinu potovu za wapinzani dhaifu.

Biashara na elimu yake ni baadhi ya vitu ambavyo wametumia kumpiga vita.

Kinachowafurahisha wafuasi wake ni jinsi Gavana Joho huepuka mitego ya wanaotaka kumzamisha kisiasa.

Joho huwapa majibu komavu na kuwaacha wakipanga mbinu mbadala za kumshutumu.

Mwanachungwa huyu huwa hatumii matusi kwa wanasiasa wenzake kama ilivyo desturi ya viongozi wengine nchini.

Kiongozi huyu anajua umuhimu wa nchi moja isiyokua na unyakuzi wa mashamba, ugavi wa raslimani kiholela, ubadhirifu wa pesa za umma na maovu mengineyo yanoyoshuhudiwa humu nchini.

Kwa kweli, jabali la Mombasa halitikisiki. Haya mawimbi ni mbolea kwa ukuaji wake. 

Joho amekua jijogoo ambalo lastahili kuwika sio Pwani tu bali Kenya nzima.