Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar ameshikilia msimamo wake kuwa atawania kiti cha ugavana katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 licha ya kupata shinikizo ya kujiondoa kuwania kiti hicho kinachoshikiliwa na Joho.
Kulingana na habari kutoka kwa Seneta Hassan Omar anasema kuna watu wengi wametumwa kwake, wengine hata na pesa ili kumshawishi ajitoe katika kinyang’anyiro hicho lakini amekariri kuwa atakuwa azma yake haitofifia. Seneta huyo ameonekana siku za hivi majuzi akikashifu serikali ya kaunti ya Mombasa inayoongozwa na gavana Joho akisema kuwa haina miradi yoyote ya maendeleo.
Aidha hiyo jana akihutubia kongamano la viongozi wa vijana katika hoteli moja mjini mombasa, Omar aliwashauri vijana kujitokeza ili kuwania viti mbalimbali za uongozi bila ya kuogopa mtu yeyote.