Wezi waliovunja na kupora bidhaa na pesa  kutoka duka la mhubiri mmoja katika kijiji cha Kiamiteng’I, lokesheni ya Mochenwa kaunti ya Nyamira,wamepewa siku kumi kujitokeza na kuomba msamaha kabla wanakijiji hao kuchukua mkondo mwingine.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanakijiji hao waliokuwa na hasira, wakiongea hiyo jana walipokuwa na mkutano wao nje ya duka hilo eneo la Kiamiteng’i , wamewapa wezi hao siku kumi  kwa kuwa wamechoshwa na vitendo vya wezi hao.Wezi hao walitekeleza uhalifu huo siku ya Jumatatu wakati waliiba shilingi zaidi ya elfu kumi na bidhaa kama mchele gunia Mbili,sukari gunia, miongoni mwa bidhaa zingine.

Mhubiri Alfred Mose amesema wezi hao wamemrudisha nyuma  kwa kuwa duka lake ndilo  analitegemea kwa kujiendeleza kimaisha.

”Duka hili langu limekuwa la kiinua mgongo kwangu kwa kuwa kile kidogo ninachokipata kinanisaidia sana lakini wakati watu wanapokuibia wanakurudisha nyuma kimaendeleo,”alieleza Mose.  

Mzee wa kijiji Nyakwana Orogo ambaye alimwakilisha chifu wa eneo hilo walikubaliana kwa pamoja ,wezi hao wasipojitokeza  sheria itachukua  mkondo wake.”Wezi wamekuwa wakitusumbua kwa muda mrefu  nasi tumekuwa tukiwaonya wenye mkono mrefu lakini sasa siku zao arobaini zimefika “alisema Nyakwana.

Kilichowashangaza wakaaji hao ni kuwa kwa bahati mbaya wezi hao walisahau koti na fimbo yao ndani ya duka hilo, kitu kiliwafanya wanakijiji  hao kupiga kura ili kubaini mwenye koti na mwenye fimbo.Mkutano huo ambao ulikuwa na watu zaidi ya 50 walipopiga kura kwa njia ya kuandika kwa vijikaratasi kura zilimwendea mshukiwa mmoja kwa asilimia 70 % kilichowapelekea kumwomba ili ajitokeze na kutaja  wengine.

“Ilitubidi tupige kura ili kubaini mwenye koti na fimbo  kwa kuwa vitu hivyo ni vya washukiwa hao”alielezea Nyakwana .Aliongezea kuwa wasipojitokeza chifu wa eneo hilo Magara Makori na naibu wake watashrlikiana  na wazee wa kijiji  nakutafuta njia ya kuwanasa washukiwa hao.

Vile vile vijana wote katika  eneo hilo wameombwa  kujiepusha na uhalifu wa aina yoyote na kuwa mstari wa mbele kuwaripoti  wenzao wanapofanya uhalifu ,pia wameombwa kujihusisha na kazi hasa za mikono ili kujiendeleza kimaisha .