Mwenyekiti wa Chama cha ODM Kaunti ya Mombasa Mohammed Hatimy, amemkosoa Seneta wa Mombasa Hassan Omar kwa kuendelea kumkashifu Gavana Hassan Joho.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza kwenye hafla ya kutoa mikopo kwa makundi ya vijana katika uwanja wa Tononoka, Hatimy alisema lazima viongozi wawe na mipango pamoja na maono ya siku za usoni.

Kauli ya Hatimy inajiri baada ya Seneta Omar kusema kuwa Gavana Joho amekosa muelekeo kwa kuwa anazingatia mwaka wa 2022 ilhali bado hana nafasi ya mwaka 2017.

Wakati huo huo, Hatimy amesema kuwa nia ya ODM kuhakikisha Joho anawania urais mwaka wa 2022 ipo, na itaendelea hadi ndoto hiyo ya kuwa na rais wa kwanza nchini kutoka eneo la Pwani imekamilika.

“Tutaendelea kumpigia debe Gavana Joho kuhakikisha anakuwa rais wa kwanza kutoka eneo la Pwani,” alisema Hatimy.

Haya yanajiri baada ya Seneta wa Mombasa Hassan Omar kuonekana kukashifu uongozi wa Joho kwa kile alichokitaja kama kushindwa kutekeleza matakwa ya wakaazi wa Mombasa.