Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baadhi ya viongozi wa kisiasa kutoka eneo la Pwani wamewashtumu wale wabunge ambao wamejiunga na chama cha Jubilee wakati Rais Uhuru amekuwa katika ziara ya wiki nzima katika eneo hilo na kuwataja kuwa wa kujitakia makuu.

Wanasiasa hao, wakiongozwa na Suleiman Dor ambaye ni mbunge wa Msambweni, viongozi hao walishangaa ni vipi serikali kupitia kwa viongozi wake wamekuwa wakizuru maeneo yanayoaminika kuwa ya chama cha upinzani na kuwashawishi baadhi ya viongozi wa kisisa wa maeneo hayo na kuijiunga na upande wa chama cha Jubilee.

Dor amewaonya viongozi hao kuwa wasitarajie kuwa kuhama kuingia katika chama cha JAP kutawapa umaarufu wa kushinda kura katika uchaguzi mwingine ujao badala ya matarajio yao alisema wengi wao watashangaa kupoteza viti.

Wabunge hao waliwataka wenzao ambao wameonyesha imani na chama cha Cord kuendelea kuonyesha imani kwa chama hicho chao ili wawe na mbinu mwafaka ya kujipanga katika uchaguzi mkuu ujao ili kushinda.

Wanapoendelea kulalamika, baadhi ya wabunge ambao tayari wametangaza azima yao kwa kuunga mkono upande wa serikali ni pamoja mbunge wa Likoni Mwahima Masoud Mwalim, Gedion Mung’aro, mwakilishi wa wanawake kutoka Kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga, mbunge wa eneo bunge la Lungalunga Hatib Mwashetani pamoja na wanasiasa wengine.