Mbunge wa Nakuru Magharibi Samwel Arama amekashifiwa na chama chake kwa kujihusisha na mrengo wa Jubilee.
Akiongea kwa njia kwa njia ya simu Ijumaa, mwenyekiti wa ODM tawi la Nakuru Peter Osono alisema Arama anafaa kutangaza msimamo wake rasmi kisiasa na wala si kujihusisha na mirengo yote.
“Arama leo yuko hapa kesho ako pale. Hio ni siasa gani? Kama amehama ODM atangaza rasmi na kujiuzulu,” Osono alisema.
Mwenyekiti huyo alikuwa akizungumza baada ya Arama kuzungumza kwenye mkutano wa rais na kuunga mkono mrengo wa Jubilee.
“Sisi hapa tuko barabara moja, na hiyo barabara ni mrengo wa Jubilee,”Arama alisema Alhamisi wakati wa ziara ya rais Nakuru.
Osono alisema mrengo wa ODM haumtambui tena mbunge Arama.
“Ako Jubilee, hatumtambui tena lakini ajiuzulu agombee tena na alikoenda,” Osono alisema.