Share news tips with us here at Hivisasa

Seneta wa Kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi amewasuta baadhi ya viongozi wa upinzani ambao alisema wanaeneza uvumi kuwa serikali ya Jubilee inafanya kampeni ya uchaguzi mkuu ujao kuwa serikali hiyo ipo katika harakati za kutimiza yale iliweza kuwaahidi raia mwaka wa 2013.

Vumbi amewashtumu viongozi wa chama cha upinzani cha Cord kwa kuendelea na mipango yao aliyoitaja kuwa na lengo la kuhujumu utaratibu wa serikali ya Jubilee kuwatimizia wakazi ahadi za serikali.

Aidha, alliwataka kuacha porojo na kujihusisha na siasa za kujenga na kuunganisha Kenya, badala ya kuendelea na siasa za kugawanya nchi kwenye misingi ya kimaeneo na kikabila.

Akizungumza katika eneo la Shika Adabu, eneo bunge la Likoni kwenye katika hafla ya rais Uhuru Kenyatta kuwapokeza wenyeji hatimiliki za ardhi ya eneo la Waitiki, Sonko alisema kuwa wanasiasa wengi wa chama cha upinzani wamekuwa wakitafuta njia za kupata umaarufu kupitia kwa matamshi ya kupinga kila hatua ya kimaendelea serikali inajaribu kufanikisha.

Sonko aliwataka viongozi wa siasa kufanya maendeleo na kuacha siasa za kupakama matope, huku ikizingatiwa kuwa wakati wa kupigwa kwa kura bado uko mbali.