Kanisa la ACK nchini Dayosisi ya Mombasa limepiga marufuku siasa ndani ya kanisa yoyote eneo la Pwani huku uchaguzi mkuu wa 2017 ukizidi kukaribia.

Share news tips with us here at Hivisasa

Askofu wa eneo hilo Julius Kalu alisema hayo huku tukitazamia uchaguzi mkuu, wanasiasa wengi eneo hilo wataanza kujumuika makanisani wakijifanyaia kampeni badala ya kuingia hapo kwa minajili ya kuomba Mungu.

Alisema wanasiasa hawafai kuruhusiwa kufanya hivyo kusukuma ajenda zao za kisiasa wakati huu wa uchaguzi.

Aidha amesema kuwa sharti mahali patakatifu lazima paheshimiwe na kupewa hadhi inayostahili.