Ingawa asimilia 37 ya wakaazi wa Mombasa ni maskini, baadhi yao ni mabwanyeye wanaomiliki kiasi kikubwa cha mali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baadhi ya matajiri wanaonena na kusikizwa upande huu wa bahari ni:

Ashok Doshi

Mfanyabiashara huyu ni mojawapo wa mabilionea wa Pwani. Kiwango chake cha pesa kilijulikana baada ya masaibu ya benki ya Imperial kuwekwa wazi. Hatua ya kuweka benki hiyo chini ya urasibu ilipelekea Doshi kuishtaki Benki Kuu ya Kenya, kwa kutomlipa shilingi bilioni moja, alizowekeza kwenye benki hiyo.

Swale Nguru

Mombasa ina wenyewe. Huwezi taja wanaojenga Pwani bila kuliorodhesha jina la bwana huyu. Ukitaka kipande cha ardhi jijini Mombasa, elekeza maneno matamu kwa Bwana Nguru. Kando na mashamba, ana mali si haba.

Amjad Rahim

Mwekezaji huyu wa Pwani hufanya biashara kote nchini. Anamiliki miradi kadhaa katika jiji la Nairobi, eneo la Westlands. Rahim pia ni mmliki wa hoteli ya kifahari na jengo maarufu la maakazi la SkyNest.

Bi Regine Butt na Bi Akhtar Shaheed Butt

Wanawake hawa wawili ni wajane wa aliyekua mmiliki wa kampuni ya magari ya Modern Coast Express. Urithi uliozua mzozo wa kifamilia unakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni nne.

Ali Punjani

Ingawa Punjani anakumbwa na shutuma nying, yeye ni mmoja wa mabwenyenye wa Mombasa. Anamiliki mali katika sehemu kadhaa Africa na pia Uingereza. Baadhi ya biashara anazomiliki ni pamoja na Hoteli ya Sun n Sand, Rising Star Commodities, Punjani Electrical Limited na Nyali International Hotel. Punjani awewekeza katika biashara nyingi sana ukiamua kuzitaja zote jua litachomoza na litue bila kumaliza.