Mwanasiasa aliyewania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira Victor Swanya Ogeto amesema hazina ya pesa ianzishwe ili wanafunzi wa familia maskini na mayatima wasaidike kimasomo katika eneo hilo.
Akizungumza siku ya Jumanne katika shule ya msingi ya Sengera iliyoko katika eneo bunge hilo la Swanya alisema hazina ya pesa ikianzishwa katika eneo hilo wanafunzi maskini watanufaika kwa kulipiwa karo ya shule.
“Wanafunzi ni wengi ambao wametoka katika familia maskini na mayatima katika eneo bunge hili watapat usaidizi wa karo baada ya hazina hii kuanzishwa, na wataendelea na masosmo yao,” akasema Swanya.
Viongonzi wa Kaunti ya Nyamira wameombwa kujumuika pamoja na kutengeneza hazina hiyo ili viwango vya masomo viinuliwe juu.
Kwa upande mwingine wakaazi wa wadi ya Rigoma iliyoko eneo bunge hilo walifurahishwa na matamshi ya Swanya kwa kusema hazina itengenezwe ambayo itawasaidia wanafunzi wengi haswa kimasomo.
“Nampongeza Swanya kwa ombi lake la kutengeneza hazina hiyo ili wanafunzi wetu wanufaike kwa kulipiwa karo. Ikiwa viongonzi na wahisani wengine watajiunga pamoja na kuunga mkono ombi lake,”alihoji Susan Ondicho mkaazi wa eneo hilo.
Aidha, wakaazi hao wamewaomba viongonzi wengine haswa wale wamo mamlakani kuiga mfano wa mwanasiasa huyo Swanya kwa kuwafadhiri wanafunzi mayatima na maskini ili masomo yainuke katika eneo hilo.