Huduma za usafiri zilitatizwa kwa mda siku ya Jumamosi katika kivukio cha feri Likoni baada ya moja ya feri zinazohudumu katika kivukio hicho kukumbwa na hitilafu za kimitambo. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Feri ya Mv Kwale ililazimika kuegeshwa pembeni kwa mda kwa ajili ya ukarabati wa dharura mwendo wa saa tano mchana. 

Hitilafu hio ilitatiza shughli za usafiri kutoka ardhi kuu hadi kisiwani baada ya tatiozo hilo kudumu kwa takribani masaa manne.

Aidha, hakuna mtu aliyeripotiwa kuumia kufwatia msongamano uliyosababishwa na hitilifu hio, huku wahudumu katika kivukio hicho wakijizatiti kuhakisha hali iko shwari licha ya changamato kama vile kuwepo na idadi kubwa ya wasafiri.

Tukio hilo linajiri wiki chache baada ya katibu mkuu katika sekta ya usafiri nchini Bw. Irungu Nyakera kubainisha kuwa kivukio cha Mtongwe feri kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo mwezi Desemba, huku feri nyingine ikitarajiwa kuwasili katika miliki ya shirika la feri ya likoni hapo mwakani. 

Hili linatarajiwa kutatua matatizo yanayoikumba shirika hilo upande wa uchukuzi katika kivukio hicho.

Kivukio hicho kinatumiwa na zaidi ya watu 300,000 na magari 6,000 kwa siku, idaidi inayotarajiwa kukuwa siku za usoni kutokana na ongezeko la watu katika eneo la Likoni.