Wizara ya kilimo, ufugaji na uvuvi imenzisha mpango wa kuwachanja mbwa na paka katika kaunti ya Nakuru.
Akizungumza afisini mwake, afisaa mkuu katika wizara hiyo Purity Muritu alisema kuwa zoezi hilo la kuwachanja mbwa na paka linajiri siku mbili baada ya mbwa wawili wenye kichaa cha mbwa kusemekana nusra waume watu katika eneo bunge la bahati.
Muritu ameongeza kuwa watu ambao wanafuga mbwa na paka wajitokeze au wawasiliane na afisi hiyo ili wanyama hao wapate chanjo.
Isitoshe afisaa huyo amesisitiza kuwa chanjo hiyo inayochanjwa mbwa na paka haina malipo yoyote, hivyo basi akasema kuwa wanashirikiana na polisi kuona kuwa maeneo bunge yote 11 ya kaunti ya Nakuru yako salama.
Aidha ametahadharisha wenye mbwa na paka kuwafungia, la si hivyo mbwa ambao wanarandaranda ovyo, watauawa ili kuzuia tishio la mbwa ambao huenda wana ugonjwa ya kichaa cha mbwa kuwadhuru binadamu.
Hata hivyo afisaa mkuu huyo amesema kuwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni hatari kwani mbwa mwenye kichaa anapomwuuma mtu, humsababishia kifo au hata kichwa kuruka.