Wanahabari mjini Naivasha wa hofu baada ya mmoja wao kuripotiwa kutoweka.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanahabari Jack Marwa ambaye alikuwa akiripotia kituo cha redio cha Hope FM alitoweka na familia yake inasema haijui aliko. Kulingana na marafiki wa mwanahabari huyo alionekana mara ya mwisho mwezi Disemba mwaka uliopita.

“Alikuwa tu mcheshi siku hiyo. Mara ya mwishokumuona ilikuwa sikukuu ya Jamhuri,” Mwanahabari mmoja alisema siku ya Jumatatu. Aidha familia hiyo imesema kuwa tayari polisi wamefahamishwa kuhusiana na kisa hicho na kuahidi uchunguzi.

Juhudi za kuzungumza na OCPD wa eneo ili ili kudhibitisha kuripotiwa kwa kisa hicho hazikufaulu kwani hakuwa ofisini.

 Nduguye Marwa, John Mwakibe, alisema kuwa wamekuwa kwenye vituo mbalimbali lakini hawajapata lolote.