Hofu ilitanda kwenye eneo la Njokeria, Njoro karibu na chuo kikuu cha Egerton baada ya wanafunzi wawili waliokuwa wapenzi kuuawa. Hayo yalitokea baada ya jamaa kumdunga kisu mpenzi wake mara kadhaa na kufariki.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Majirani waliokuwa na ghadhabu walimshambulia jamaa huyo na kumuua.

Aidha inaarifiwa mwanaume huyo alitekeleza mauaji hayo baada ya mzozo wa kimapenzi.

“Wawili hao walikuwa wapenzi. Inaarifiwa msichana huyo alifika nyumbani usiku na mpenziwe kushuku alikuwa na uhusiano na jamaa mwingine,” Alfonce Otieno alisema.

Miili ya wawili hao ilichukuliwa na kupelekwa kwenye ufuo wa hospitali ya Egerton.