Profesa Thomas Karua, kutoka Chuo kikuu cha Pwani, ameelezea wasiwasi kuwa huenda viwango vya umasikini katika eneo la Pwani vikaongezeka maradufu siku za usoni kufuatia kushuhudiwa kwa idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na ajira.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Alhamisi, Prof Karua alisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona kuwa idadi kubwa ya vijana hawana ajira eneo la Pwani, ikizingatiwa wao ndio wazazi wa siku za usoni.

Alisema kuwa hali hiyo imewasababisha vijana hao kurandaranda mijini na kuishia kujihusisha katika visa vya uhalifu.

“Ningependa kuzihimiza serikali za kaunti pamoja na ile ya kitaifa kuhakikisha kuwa vijana wanapata ajira kwa kuwa wanapitia shida nyingi maishani,” alisema Karua.

Aidha, aliongeza kuwa iwapo vijana watapewa ajira, idadi ya visa vya ugaidi huenda vikapungua pakubwa.