Zaidi ya asilimia 40 za hoteli katika kanda ya Pwani zimelazimika kufunga kutokana na ukosefu wa wateja huku idadi ya watalii ikipungua kwa kiasi kikubwa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha wahudumu wa hoteli Mombasa Sam Ikwaye, idadi ya watalii hupungua kuanzia mwezi wa Aprili hadi mwezi wa Julai kwa asilimia 80 ya watalii.

Ikwaye amesema kuwa watalii kutoka nchi ya Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na italia hupendelea kutembelea nchi ya Usheli katika msimu huu.

Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akihutubia wahudumu wa hoteli katika kongamano la kuwahamasisha kuhusu njia mbadala ya wahudumu kufanya biashara liloandaliwa katika hoteli moja jijini Mombasa siku ya Jumatano sasa amependekeza wahudumu wawe na biashara za kando ili kujikimu kimaisha.