Wasafiri katika kivuko cha feri cha Likoni. [Picha/ nation.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la KFS Bakari Goa amesema kuwa shughuli za usafiri katika kivuko cha Mtongwe zimeathirika kufuatia kuharibika kwa feri mbili.Akizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi, Goa aliwataka wakaazi wa Mtongwe kuwa na subira wakati feri hizo zinapofanyiwa marekebisho.“Kuweni na subira wakati huu ambapo tunafanyia feri hizo marekebisho,” alisema Goa.Hata hivyo, alisema kuwa feri hizo zinatarajiwa kuanza kuhudumu tena wiki ijayo.Goa alisema kuwa hatua hiyo ndiyo iliyosababisha msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Likoni nyakati za asubui na jioni.Kwa sasa, feri tatu pekee ndizo zinazohudumu katika kivuko hicho.Goa alisema kuwa feri mpya ya MV Safari iliyotarajiwa kufika nchini mwezi huu na kusaidia katika kupunguza msongamano katika kivuko hicho itawasili pindi tu kesi kuhusiana na ujenzi wa feri hiyo itakapokamilika.“Feri mpya itawasili hivi punde baada ya mahakama kutoa uamuzi wake mwezi huu,” alisema Goa.Wakati huo huo, idara ya usalama Kaunti ya Mombasa imeanzisha ukaguzi wa mizigo na magari katika kivuko cha Likoni kama njia mojawapo ya kuboresha usalama kwa watumizi wa kivuko hicho.Akizungumza katika kivuko hicho cha Likoni, Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki aliwataka wanaotumia kivuko hicho kushirikiana na maafisa wa usalama wanaoshika doria eneo hilo ili kuwarahisishia kazi yao.“Tunahitaji ushirikiano mwema baina ya maafisa wa polisi na wasafiri ili kuimarisha usalama katika kivuko hiki cha Likoni,” alisema Achoki.