Sehemu ya kivukio cha Mtongwe. [Photo/ nation.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Huduma katika kivuko cha Mtongwe ferry zimerejea baada ya kusitishwa kutoka mwezi wa Oktoba mwaka Jana.Huduma hizo sasa zitatekelezwa kwa zamu, ya kwanza ikiwa kutoka alfajiri hadi saa nne asubuhu, huku ya pili ikiwa ni kutoka saa kumi alasiri hadi saa nne usiku.Mkrugenzi mkuu wa huduma za ferry nchini Bakari Gowa amewaomba msamaha wakaazi wa Mtongwe kwa mahangaiko waliopitia kwa muda ambao huduma hizo zilikuwa zimesitishwa.“Tunaomba msamaha kwa vile muliteseka sana kwa kipindi hicho chote lakini sasa hali ya usafiri iko shwari,” alisema Gowa.Aidha, Gowa ametoa hakikisho kwamba watafanya kadri ya uwezo wao ili kufanikisha huduma hiyo.“Tutajitahidi kila tuwezalo kuhakikisha kuwa wasafiri wote wanahudumiwa vyema,” alisema Gowa.Huduma za ferry ya Mtongwe zilizinduliwa upya mwaka jana na Rais Uhuru Kenyatta baada ya shughuli katika kivukio hicho kusitishwa kwa zaidi ya miaka 20 kutokana na mkasa uliotokea ambapo Mv Mtongwe ilizama na watu zaidi ya mia mbili kuangamia.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6