Huku uchaguzi mkuu ujao ukizidi kupiga hodi, mirengo mikuu ya kisiasa nchini; Jubilee na Cord, imejitosa katika kampeni za mapema ili kuwahi umaarufu kati ya wafuasi kwao. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kila mrengo umebuni mbinu yake ya kuziuza sera zake, chaguo ambalo linaathiri pakubwa idadi ya kura kila mrengo utavuna kutoka kwa wananchi. 

Jubilee imejizatiti kumaliza ahadi iliyowapa wananchi. Hili huenda likawa mvuto mkubwa zaidi katika azma yao ya kuwauzia wananchi sera za hatamu itakayokuja. 

Kwa upande wao, Cord wameonyesha mgawanyiko kwa kukosa kuafikiana kuhusu kiingozi anayefaa kwa wale waliopo watatu. 

Kuharibia zaidi, Cord wameanika tofauti zao kwa wananchi, kuonyesha ukosefu wa ukomavu wa kutoa suluhu kwa mizozo ya ndani. 

Kinara mkuu Raila Odinga na wenzake Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka wameonyesha azma yao kila mmoja kuwania kiti cha urais. Hii inamaanisha kuwa kura za eneo la ukambani huenda zikajitenga na debe la Raila na Wetangula, kama za eneo la Magharibi, huku kura za Nyanza nazo zitajitenga na debe za Wetangula na Kalonzo. 

Hilo likitimia, Jubilee itafurahi ushindi wa mapema wa kuunganisha kura za Bonde la Ufa na Kati. Hili litaashiria taswira mbaya ya juhudi za Cord kuikosoa serikali.

Ikiwa wana haja ya kushinda, wanafaa kuweka tofauti zao kando na kuzidi kuwahamasisha wananchi kuhusu makosa ya Jubilee na kutafuta kiongizi mwafaka kati yao watatu.