Ziara ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto katika eneo la Kisii imeonekana kuzaa matunda na huenda ikaupiku muungano wa Cord katika ngome yao ifikapo uchaguzi wa mwaka ujao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni baada ya Rais Kenyatta kutangaza kuwa serikali ya kitaifa itawafidia wakimbizi wa ndani kwa ndani katika eneo la Gusii hivi karibuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo nzima la Kisii

Kulingana na maoni yangu huenda wakimbizi wakifidiwa itakuwa hakikisho kubwa kwa serikali ya Jubilee kupata kura nyingi zaidi kutoka eneo la Kisii kuliko zile walipata katika uchaguzi uliopita.

Pia Rais Kenyatta alianzisha miradi tofauti tofauti katika eneo hilo haswa katika sekta ya afya na ukarabati wa barabara katika maeneo tofauti tofauti jambo ambalo huenda Jubilee itatumia katika kudhibiti umaarufu wa muungano wa Cord  katika eneo zima la Gusii.

Na ikiwa Jubilee haitashinda muungano huo wa Cord katika eneo la Kisiii kwa kunyakuwa kura nyingi katika eneo basi huenda Jubilee ipunguze kura za muungano wa Cord kuliko zile walizopata katika uchaguzi uliopita.