Lango la kampuni ya kusambaza maji katika mkoa wa pwani. [Picha-NMG]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Muungano wa wafanyikazi wa hoteli kaunti ya Kilifi wameonya kuwa zaidi ya hoteli 40 mjini Malindi na Watamu  huenda zikafungwa iwapo huduma ya maji haitaweza kurejeshwa hivi karibuni.

Kwa sasa zaidi ya watu milioni moja wanaoishi Mombasa na Kilifi wanahangaika kwa sababu ya ukosefu wa maji kufuatia kukatizwa kwa huduma za umeme katika kituo cha maji cha Baricho kwa muda wa  zaidi ya wiki moja iliyopita.

Tarehe 19 mwezi huu, kampuni ya kusambaza umeme ilikatiza huduma za umeme katika kituo cha Baricho baada ya kampuni ya kusambaza maji ya mkoa wa pwani kukosa kulipa deni la shilingi bilioni 60.

Kufuatia hatua hiyo, idadi ya wakaazi milioni 1.5 wa Mombasa na Kilifi, viwanda, hospitali na hoteli vimekosa maji .

Stesheni ya Baricho  inategemewa sana na wakaazi wa Kilifi na Mombasa kwa sababu hutoa lita milioni 90 ya maji kila mwaka. 

Katika lita milioni 90 ya maji, kampuni ya kusambaza maji eneo la pwani hutoa lita milioni 40 ya maji kila siku.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kusambaza umeme eneo la pwani Hezekiah Mwalala alisema kuwa kutolipa kwa deni hilo kumeathiri huduma zake kwa sababu ya kukosa fedha za kulipia huduma mbalimbali za kampuni hiyo