Jamii ya Ogiek katika kaunti ya Nakuru imekataa pendekezo la serikali kutumia ekari 17,000 kwenye msitu wa mau kuwapa makao maskwota.
Zaidi ya wakaazi 700 wa jamii hiyo kutoka maeneo ya Soget na Londiani wamesema kuwa wanafurahia ekari 5,000 za ardhi ambazo wamekuwa wakitumia tangia zama.
Wakiongozwa na Francis Maritim ambaye ni mwenyekiti wa jamii hiyo ya Ogiek, wanajamii hao wamesema kuwa serikali inafaa kuweka bayana swala hilo ili kuzuia uhasama baina ya jamii zinazokaa karibu.
“Tumekuwa tukitafuta haki yetu mahakamani, na hatuoni haja ya kuhamishwa kutoka ardhi tunamokaa hadi nyingine. Siku za usoni tunahofia vita vya kijamii ikiwa serikali itafanya hivyo,” alisema Maritim.