Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutia sahihi mswada wa kisheria, 2015.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Sheria hiyo inalenga kuwezesha wakenya kupata haki kwa njia rahisi na haraka bila kuzingatia hali yao ya kifedha.

Sheria hiyo, ambao tayari imeidhinishwa na bunge la kitaifa, inamwezesha mwananchi wa kawaida kupata wakili atakayelipwa na serikali kumwakilisha kwenye kesi iwapo atashindwa kuhumudu malipo ya wakili.

Afisa wa mipango kutoka shirika la International Commissions of Jurists (ICJ), Steve Ogolla amesema kutajengwa vituo vya kisheria kwenye kaunti zote arobaini na saba kuwawezesha wananchi kupata ushauri wa kisheria baada ya rais kutia sahihi sheria hiyo.

“Sheria hii itabadilisha mkondo wa kutoa huduma za kisheria humu nchini manake kwa sasa, ni wale walio na fedha ndiyo wanaopata huduma wanazotaka. Kupitia hii sheria, mwananchi atakuwa na ufahamu wa ni wapi atapata huduma na jinsi ya kuzipokea kwa njia mwafaka,” alieleza Ogolla.

Maswala ambayo hayatapata usaidizi wa kisheria chini ya sheria hiyo ni pamoja na kukwepa kulipa kodi, kumuharibia mtu jina na mizozo ya madeni.