Hali ya uzuni ilitanda katika uwanja wa michezo wa Jomo Kenyatta jijini Kisumu, wakati mwili wa Fidel Odinga, mwanae Raila Odinga ulipowasili.

Share news tips with us here at Hivisasa

Maelfu ya waombolezaji walimiminika katika uwanja huo na kugubikwa na majonzi, wakati wa kuutazama mwili wa mwenda zake aliyeaga wiki iliyopita.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, aliyekuwa mbunge wa Westandlands Fred Gumo ameitaka serikali kuharakisha kutoa matokeo ya chanzo cha kifo cha Fidel.

Baadhi ya viongozi waliofika wameelezea kuwa kifo cha fidel si cha kawaida, na wameomba serikali kuharakisha katika uchunguzi na kubaini kilichosababisha kifo hicho.

Mwili wa mwenda zake ulissafirishwa nyumbani kwake mjini Bondo, kisha usafirishwe baadae katika boma la babake, kang’o ka Jaramogi kesho asubuhi kwa mazishi.

Marehemu alipatikana amefariki nyumbani kwani Karen, Nairobi, baada ya kuwa nje usiku mzima na marafiki.

Uchunguzi umekua ukiendelea kubaina chanzo cha kifo chake, huku mpaka sasa maafisa wa polisi wakiwa bado hawajapata majibu sahihi kwa maswali yao.