Mwenyekiti wa ICPAK Julius Mwatu katika hafla ya awali. Picha/ the-star.co.ke
Taasisi ya uhasibu nchini ICPAK imeunga mkono pendekezo la Tume ya kutathmini na kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC la kupunguzwa kwa mishahara ya wafanyikazi wa umma.
Kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatano, naibu mwenyekiti wa taasisi hiyo Julius Mwatu alisema kwamba imebainika wazi wafanyikazi wa umma humu nchini wanapata asilimia kubwa ya mapato, hatua aliyoitaja kulemaza huduma zingine mbalimbali.
Mwatu alisema kuwa sharti mishahara ya wafanyikazi hao kupunguzwa.
Mwatu aliongeza kwamba kushuhudiwa kwa migomo ya kila mara ya wafanyikazi wa umma pia kumechangia kuongezeka kwa malipo na utumizi wa kiwango kikubwa cha fedha kwa taifa, hatua aliyoitaja kudidimiza na hata kulemaza uchumi wa nchi.
Hata hivyo, alisema kuwa swala hili sio lak upuzilia mbali na endapo wafanyikazi wa umma hawatapunguzwa mishahara, basi taifa hili litapitia changamoto nyingi ikiwemo madeni kutoka kwa sekta mbalimbali.