Mwakilishi mteule wa wadi ya Molo Nakuru Beatrice Nyawira amesema kuwa idadi ndogo ya wanawake walioteuliwa au kuchaguliwa katika bunge la kaunti ya Nakuru inaathiri upitishaji wa miswada inayowahusu wanawake.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza Jumanne, Nyawira alidai kuwa ni vigumu kuwashawishi wanaume ambao ndio wengi bungeni kuunga mkono baadhi ya miswada inayowalenga wanawake pekee.

Ugumu huu kulingana naye hutokana na hatua ya wawakilishi wa kiume kutoelewa uzito wa maswala haya kama vile dhulma dhidi ya akina mama, umuhimu wa sodo au hata umuhimu wa kuweka vyoo katika soko.

Licha ya changamoto hizi nyawira alisema kuwa wameweza kupitisha miswada miwili inayogusa jinsia ya kike.

Moja ya miswada hiyo ni ule wa kutenga shilingi milioni 30 katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2015/2016 zitakazotumiwa kununua sodo ambazo zitakabidhiwa wanafunzi katika shule za msingi za umma zilizoko kwenye kaunti ya Nakuru.

Bunge la kaunti ya Nakuru lina wawakilishi wa wadi 73 huku 21 wakiwa wanawake.