Huku chanjo ya ugonjwa wa Shurua al maarufu Measles ama Ukambi na rubella ikiendelea kote nchini, kaunti ya Kisii imeandikisha idadi ndogo katika shughli hiyo jambo ambalo limesemekana kutowafurahisha madaktari kwani kaunti hiyo inalenga kuwachanja watoto zaidi ya 600,000.
Akizungumza nasi siku ya Jumatano mjini Kisii daktari Charles Ayora alisema kuwa idadi mbayo imejitokeza tangu shughuli hiyo ianze ni chache zaidi ikilinganishwa na matarajio ya wahudumu wa afya.
Ayora aliomba wazazi kutosubiri wahudumu wa afya kuwatembelea nyumbani kwao na kuwapeleka wana wao katika shule na makanisa yalio karibu nao kupata chanjo hiyo.
“Tumeshangaa sana maana Idadi ambayo tumeandikisha tangu chanjo ya ugonwa wa Shurua na Rubella inoe nanga ni chache zaidi katika kaunti yetu ya Kisii,” alisema Ayora.
“Tunaomba wazazi kuwajibika na kuhakikisha watoto hao wamepata chanjo hiyo maana chanjo hiyo ni ya maana sana kwa watoto walio chini ya miaka 14,” aliongeza Ayora.